Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii
DCC Mlimani Park Orchestra (au Mlimani Park) ni bendi ya muziki wa dansi yenye makao yake jijini Dar es Salaam, Tanzania. Bendi Ilianzishwa mwezi kama huu mnamo mwaka wa 1978. Waanzilishi wa bendi hiyo ni pamoja na Muhidin Maalim Gurumo, Abdallah gama na Abel Balthazar. Hassan Bichuka na Suleiman Mwanyiro waliingia 1982 kutokea Juwata jazz.
DCC Mlimani Park Orchestra (au Mlimani Park) ni bendi ya muziki wa dansi yenye makao yake jijini Dar es Salaam, Tanzania. Bendi Ilianzishwa mwezi kama huu mnamo mwaka wa 1978. Waanzilishi wa bendi hiyo ni pamoja na Muhidin Maalim Gurumo, Abdallah gama na Abel Balthazar. Hassan Bichuka na Suleiman Mwanyiro waliingia 1982 kutokea Juwata jazz.
Mtindo maarufu wa bendi ya DDC ni Sikinde ngoma ya ukae, yaani Sikinde Ngoma ya Nyumbani.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Mlimani Park iliundwa na kundi kubwa la wanamuziki kutoka bendi ya Dar International.
Ilianza wakat Dar International ilipokodishwa na Chuo Cha Ardhi katika sherehe yao ya kuwaaga wanachuo wa zamani na kukaribisha wapya. Chuo cha Ardhi kilikodi ukumbi wa Mlimani Park kwa ajili ya shughuli hiyo.
Wakati huo huo utawala wa Mlimani Park ulikuwa mbioni kutengeneza bendi baada ya kumalizika mkataba wa Orchestra Fukafuka katika ukumbi huo, chini ya mwanamuziki Tchimanga Assossa ambaye alikuwa amekuja na Bendi ya Fukafuka.
Assosa alibaki nchini na alikuwa katika hatua za mwisho za kwenda kufuata wanamuziki wengine kutoka Kongo kwa ajili ya ukumbi huo. Hivyo basi Dar International wakati huo ndio wakivuma na nyimbo kama Magreti walianza kuporomosha muziki chini ya kiongozi wao Abel Balthazal. Uongozi wa Mlimani Park ulipigwa butwaa na muziki wa hawa jamaa, Abel aliitwa pembeni na kuulizwa bendi iko chini ya mkataba wa nani? Na je, wanamuziki wangeweza kukubali kuajiriwa na na Mlimani Park wakati huo ikiendeshwa na TTTS?
Kwa vile Dar International ilikuwa ya mtu binafsi na hawakuwa na ajira yoyote ya kudumu katika bendi hiyo, haraka sana wanamuziki walikubali wazo hilo. Kesho yake viongozi wa Dar International walienda kukutana na viongozi wa ukumbi wa Mlimani Park, na wakakubaliana kuazisha kambi ya bendi mpya palepale katika ukumbi wa Mlimani.
Haikuwa taabu maana vyombo vilivyonunuliwa wakati wa mkataba wa Orchestra Fukafuka vilikuwa mali ya Mlimani Park kwa hiyo bendi ilianza kwa Abel kusisitiza kupata wanamuziki kama Muhidin Maalim Gurumo.
Hapo ikumbukwe kuwa ni huyu huyu Abel ambaye ndiye aliyeisuka Dar International baada ya kuwachukua wanamuziki wote wa Safari Trippers kundi zima wakati huo, kina Kassim Mponda, Joseph Bernard, Marijani Rajabu, Ben Peti, Zito Mbunda, Bito Elias na wengine kasoro Christian Kazinduki na kutoka Tanzania Stars ya Maggot walitoka Joseph Mulenga, George Kessy , Haruna Lwali na wengineo.
Na kwa staili hiyohiyo skwadi nzima ya Dar International ikageuka kuwa Mlimani Park. Muda mfupi kabla la hili ugomvi mkubwa ulikuwa umetokea Dar International kati ya Marijani Rajabu na Abel Balthazar katika ubishi kuhusu tungo aliyoleta Marijani ambayo Balthazar alidai kuwa ni ya Tabu Ley kwa hiyo akatunge tena, jambo lililoleta kushikana mashati, na kusababisha Marijani kusimamishwa kazi.
Wakati yuko benchi ndipo mpango mzima wa kuhamia Mlimani ulifanyika hivyo mwenye vyombo alilazimika kumfwata tena Marijani na kumwomba aunde bendi upya, na ndipo Super Bomboka ikaundwa.
Mlimani Park ikaanza ikiwa na Tchimanga Assossa ambaye safari ya kwenda kutafuta wanamuziki Kongo ikawa imekwisha.
Na mchango wa kudumu wa Assossa wakati huo ni utunzi wa ule wimbo Gama.
Muhidin Maalim Gurumo, Hassani Bitchuka, Abel Balthazar, "King" Michael Enoch, Cosmas Thobias Chidumule, Shaaban Dede, Maalim Khamis Kinyasi, Max Bushoke, Ramadhan Mwinyikondo, Hussein Jumbe, Henry Mkanyia, Julius Mzeru, Joseph Mulenga na Suleiman Mwanyiro
Mpiga rythim guitar Abdallah Gama (kushoto) na mpiga solo Shabani Yohana Wanted
Wapiliza saxphone wa Sikinde
Kutoka kushoto ni Hussein Jumbe, Abdallah Kinguti, Benno Villa Anthony na Hassan Rehani Bitchuka
![]() |
Muhidin Maalim Gurumo na Hassan Rehani Bitchuka |
Wapuliza trumphet wa bendi ya Mlimani Park, Mbaraka Othman (kushoto) na Hamisi Milambo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...