Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino
Mlowola amesema njia nzuri ya kusambaza na kupeleka ujumbe kwa wananchi
kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ni kutumia sanaa.
Mlolowa
amesema hayo wakati wa uzinduzi wa filamu inayojulikana kwa jina la
BAHASHA iliyoandaliwa na ubalozi wa Uswisi na Uholanzi kwa kushirikiana
na Takukuru inayozungumzia madhara yanayojitokeza katika sehemu
mbalimbali inayosababishwa na rushwa.
Akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, Mlolowa amesema sanaa ni
njia nzuri ya kuweza kufikisha ujumbe kwa urahisi kwakuwa wananchi
wanapenda sana sanaa na filamu hii itawasaidia zaidi katika kuona
madhara yanayokuja baada ya rushwa.
Amesema kuwa, filamu hii ina
ujumbe mzuri sana na wanatarajia mwakani katika mbio za mwenge isambazwe
ili nchi nzima ili wananchi waelewe madhara yatokanayo na rushwa na
wananchi wameipokea kwa muitikio mkubwa sana.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlolowa akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana usiku Jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa Filamu hiyo Louise Kamin akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana, filamu hiyo inayohusu Rushwa imewezwa kuandaliwa baina ya ubalozi wa Uswisi na Uholanzi pamoja Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).
Waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini filamu ya BAHASHA iliyozunduliwa jana usiku na Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...