Kuhusu BROKEN HEART: Hakuamini mahusiano yake na mtu aliyempenda yaishe kwa yeye kudumbukizwa kwenye dimbwi la msongo wa mawazo, aliyempenda aligeuka kuwa adui.
'Mapenzi ni kitu ambacho kinaweza kukufanya chizi, sihitaji tena mwanaume maishani mwangu.' Alizungumza.
Lakini maisha ni safari, na akiwa katika safari ya maisha alijikuta akizama kimapenzi kwa mwanaume mwingine, mwanaume aliyedhani ni tofauti na waliopita.
Shilole A.K.A Shishi Baby Kulia akiwa pamoja na Jackson  Fute kuzindua rasmi riwaya waliyoandika pamoja inayokwenda kwa jina la Broken Heart, uzinduzi huo ulifanywa ndani ya Duka la vitabu la Mak Books and Brains Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Bwana Jackson Fute (Kushoto) akiongea na waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua riwaya waliyo andika na Shilole.
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Bongo Movie na sasa Mtunzi wa vitabu Bi. Zena Yusuf Mohamed Maarufu kwa jina la Shishi Baby, akielezea kwa ufupi namna alivyopata wazo la kuandika Riwaya ya Broken Heart kuwa inalenga historia yake ya kweli kabisa na kuongeza kuwa amefurahi kumshirikisha mwandishi chipukizi Bw. Jackson Fute na kazi imeenda vizuri. pia aliwaomba watanzania wamuunge mkono kwani kitabu kinauzwa kwa Tsh 15,000 tu na Online Ebook ni Tsh 3,000 kinapatikana kote Duniani. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...