*Ni baada ya mtaji wake kutetereka, yapewa siku 90 kujitathimini

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BOT) imeamua kuchukua usimamizi wa Bank M kuanzia leo na uamuzi huo unachukuliwa baada ya kubainika benki hiyo ina upungufu mkubwa wa ukwasi.

Akizungumza leo Dar es Salaam Gavana BoT Profesa  Florens Luoga amesema kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha Sheria namba 56 (1)(g)(III)cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 ameamua kuchukua uamuzi huo kwa Benk M na sasa itakuwa chini ya usimamizi wa BoT.

"Upungufu huu wa ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa Bank M kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake,"amesema Profesa Luwoga.

Amefafanua kutokana na uamuzi huo ,Benki Kuu imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Bank M kuanzia leo(Agosti 2) mwaka huu na kutokana na uamuzi huo BoT imemteua Meneja Msimamizi atakayesimamia shughuli za benki hiyo kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi.

Ameongeza Watanzania wafahamu kuwa katika kipindi kisichozidi siku 90 kuanzia leo , shughuli zote za utoaji wa huduma za kibenki za Bank M zitasimamiwa ili kuipa nafasi BoT kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

P ia kuwa BoT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Florens Luoga (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya Benki Kuu kuchukua usimamizi wa Bank M Tanzania Plc (Bank M) kutokana na upungufu mkubwa wa ukwasi kwa benki hiyo, kulia ni Naibu Gavana wa Uthabiti wa sekta ya Kifedha, Dkt. Bernard Kibesse na kushoto ni Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...