Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeridhia ombi la uunganishwaji wa benki za Benki ya Wanawake Tanzania(TWB) pamoja na TPB Bank Plc.

Kutokana na hatua hiyo sasa kutakuwa na benki moja kuanzia Agosti 3 mwaka huu itakayoendelea kuitwa benki ya TPB Bank Plc ambayo itaendelea kuwa na mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florenc Luoga amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na ombi la wanahisa la kutaka kuunganishwa kwa benki hizo. Amesema hivyo kuanzia sasa wateja, wafanyakazi , mali a madeni yote ya TWB yataunganishwa na yale ya benki ya TPB huku akifafanua muunganiko wa benki hizo unaifanya benki ya mpya ya TPB Bank Plc kuwa imara zaidi na itakuwa ina mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa chini ya kifungu cha 17 cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha.

"Benki Kuu inawaomba wateja wa benki ya TWB kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mpito cha uunganishwaji wa benki hizi na watendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaotolewa na menejimenti ya uongozi wa benki ya TPB,"amesema Profesa Luoga. Wakati huo huo amesema Benki za TOBACO na KCBL kwa sasa zimeweza kuongeza mtaji na kukidhi kiwango kinachohitajika kisheria na hivyo zinaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Amesema BoT inawagakikisha wananchi kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha. Awali Gavana Luoga amefafanua Januari 4 mwaka huu BoT iliongeza muda wa miezi sita kwa benki tatu ambazo ni Tandahimba Community Bank Limited (TOBACO), Tanzania Women's Bank Plc(TWB) na Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

Ambapo mpaka Juni 30 mwaka huu ili kufikisha kiwango cha mtaji kinachohitajika na sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2007 na kanuni zake za kiwango cha chini cha mtaji cha Sh.bilioni mbili kwa benki za wananchi. Aidha benki hizo ziliongezewa muda wa mwezi mmoja hadi Julai 31 mwaka 2018 ili kukamilisha taratibu za kuongeza mtaji.

Kutokana na kutolewa kwa muda huo ndipo wanahisa wa TWB na TPB walipoamua kuunganisha benki hizo na BoT imeridhia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...