KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo amefanya ziara ya kushtukiza kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro wilayani Mkinga na kuridhishwa na utendaji wa watumishi hao huku akiwahaidi kupeleka maabara inayohamishika kwenye kituo hicho ili kuweza kupima dawa za malaria, ukimwi na dawa za kuulia vijidudu.
TFDA na Taasisi za serikali wanatoa huduma ya kufanya ukaguzi wa bidhaa za chakula, dawa,vipodozi, vifaa tiba na vitenganishi kwa ajili ya kuhakikisha vinaingia nchini zikiwa salama na kwamba vimeidhinishwa na mamlaka husika kabla ya kuingia nchini
Agnes aliyasema hayo wakati akiwa eneo hilo mara baada ya kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo wakati wa ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia kama watendaji waliowapa dhamana kwenye vituo vya forodha wanafanya kazi kulingana na sheria, taratibu na miongozi walizowapatia ya kikaguzi kazi kubwa inafanyika kwenye vituo hivyo
Alisema hilo linatokana na eneo hilo kutokuwa na maabara inayohamishika hivyo wataiweka ili waweze kujua dalili na bidhaa kama zinazoingia wakati zinapita mpakani ziruhusiwe au kutokuziruhusu kutokana baada ya kujiridhisha iwapo zinapaswa kufanywa hivyo .
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akionyeshwa baadhi ya taarifa kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya na mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola . mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...