Kuelekea Tanzania ya viwanda katika eneo la kilimo cha umwagiliaji, Mpango kabambe wa maendeleo ya kilimo awamu ya pili una lengo la kuimarisha kilimo cha umwagiliajiili kupunguza utegemezi wa mvua kwa kuongeza eneo la umwagiliaji nchini, kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025.
Hayo yameelezwa leo wakati wa maonyesho ya wakulima nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Mjini Bariadi na Mhandisi Ebenezer Kombe kutoka kanda ya Umwagiliaji ya Mwanza alipokuwa akiongea na wananchi waliotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mhandisi Kombe amesema kuwa ilikufanikisha hayo, serikali itashirikiana na sekta Binafsi kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga mifereji mikuu, mifereji ya kati na mabwawa ya kuhifadhia maji kwenye maeneo yenye ukame.
Aidha Bw. Kombe alisema, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kushirikiana na Halmashauri husika itahamasisha wakulima kupitia vyama vya umwagiliaji kuchangia katika ujenzi wa mifereji midogo ya kuingiza maji mashambani na kushiriki katika kuitunza mifereji hiyo.
“Tunawafundisha wakulima kuzalisha kwa tija na ufanisi kwa kutumia miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja na kulima zaidi ya mara moja kwa mwaka, kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa mfano kilimo shadidi cha mpunga (kilimo chenye matumizi kidogo ya maji).” Alisisitiza. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

picha kushoto Afisa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Petro Sarawat, akimpatia kipeperushi mwananchi aliyetembelea banda hilo katika viwanja vya nane vya Nyakadindi , Bariadi Mkoani Simiyu.
Aliyevaa shati Jeupe Meneja wa kanda ya ziwa wa kampuni ya Davis and Shirtlff akiwaonyesha wakulima vifaa vinavyotumika katika kilimo cha umwagiliaji, vinavyouzwa na Kampuni hiyo katika banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwenye viwanja vya nanenane vya Nyakadindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Picha ya Pamoja ikonyesha baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji walioshiriki maonyesho wa wakulima nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. (Habari na Picha na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Tume ya Taifa ya Umwagiliaji)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...