Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akizungumza leo Jijini Dodoma na wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (hawapo katika picha) ambapo timu ya mpira wa miguu wanawake waliibuka washindi wa kwanza, katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harrison Mwakyembe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa wachezaji walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Masharik (hawapo katika picha), wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji hao leo Jijini dodoma, kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Zanzibar Bw.Hamis Alli Mzee,anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Karate.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Bibi. Suzan Mlawi (katikati) akifurahi
pamoja na wachezaji wa mpira wa pete leo
Jijini Dodoma baada ya timu hiyo kurejea
ikitokea Bujumbura nchini Burundi ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambapo iliibuka mshindi wa pili.
(Picha na Shamimu
Nyaki-WHUSM)
Na
Shamimu Nyaki –WHUSM
WAZIRI
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa
mwanamichezo anayepaswa kujivunia mafanikio katika michezo ni yule ambaye
ameiletea nchi sifa nzuri ya ushindi.
Hayo
ameyasema leo Jijini Dodoma katika halfa ya kuzipongeza timu zilizoshiriki
mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika mjini Bujumbura nchini
Burundi ambapo timu ya mpira wa miguu ya wanawake waliibuka washindi wa kwanza.
“Sasa naona wachezaji wetu mmebadili muelekeo kwa kuweka juhudi na
kuhakikisha mnailetea heshima nchi yetu kwa kuja na kombe la ushindi, hiki ndio
kilele cha mafanikio kwa wanamichezo” alisema Dkt. Mwakyembe.
Anazidi
kueleza kuwa Serikali itaendelea kuweka
juhudi kwa timu za wanawake ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa katika michezo
kwani zimekuwa zikifanya vizuri ambapo
ndani ya muda wa miezi miwili zimeleta
makombe mawili kutoka katika mashindano ya kimataifa ikiwemo CECAFA.
Dkt.
Harrison Mwakyembe alisisitiza kuwa zama za kupeleka wachezaji kwa mazoea zimepitwa
na wakati bali wachezaji watakaokuwa wakishiriki michezo ya nje ya nchi ni wale
wenye juhudi na uzalendo kwa taifa lao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...