Na Asteria Muhozya, Simanjiro

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema kuanzia sasa Serikali itaanza kutoa Leseni za madini biashara ya madini kwa masharti magumu huku ikimtaka kila mwombaji kutoa taarifa za mauzo ya uzalishaji, usafirishaji pamoja na mnyororo mzima wa biashara ya madini ikiwemo fedha zinazoingia nchini kutokana na biashara hiyo.

Pia, ameiagiza Tume ya Madini kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kila jambo katika mnyororo huo linasimamiwa kikamilifu na kuongeza kuwa, yeye kama waziri mwenye dhamana atahakikisha anafuatilia kila hatua itakayochukuliwa na tume hiyo.

“Tume ichukue hatua. Nitakuwa na ninyi. Msiache hata mmoja atakayekwenda kinyume na haya. Nilifanya hivyo katika Sekta ya Utumishi wa Umma hata huku kwenye sekta ya madini, sitashindwa kufanya hivyo,” alisisitiza Waziri Kairuki.Waziri kairuki aliyasema hayo jana tarehe 3 Agosti, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara wakati akipokea taarifa ya Kamati Maalum iliyoundwa kuchunguza mnyororo wa madini ya vito nchini.

Kamati hiyo ilifanya kazi yake kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 26 Aprili, 2018 kwa jukumu la kuchunguza mnyororo wa madini ya vito kuanzia kuzalisha hadi usafirishaji nje ya nchi pamoja na kubaini sababu za utoroshaji wa madini na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuzuia utoroshaji.

Pia, aliiagiza tume ya madini kuanzia tarehe 4 Agosti, kuhakikisha inapata taarifa za uzalishaji za migodi yote inayozalisha huku akitaka migodi husika ieleze mahali inakouzia madini yao, anayeuziwa madini hayo na kuongeza kuwa, zoezi husika linawajumuisha pia dealers.
 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akipokea taarifa ya Kamati kutoka kwa Mwenyekiti Sam Molle (kulia). Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kushoto0) 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula akizungumza jambo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya kamati iliyochunguza mnyororo wa madini ya vito kuanzia kuzalisha hadi usafirishaji nje ya nchi pamoja na kubaini sababu za utoroshaji wa madini na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuzuia utoroshaji. Anayefuatilia kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa, Simon Msanjila.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini na wabunge wengine wa Mkoa wa Manyara, Kilimanjaro na Arusha.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Wataaalm wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini , Ofisi ya Madini Mirerani, Ofisi ya Madini Mkoa wa Arusha na Mtaalam kutoka Taasisi ya Jilojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...