NA TIGANYA VINCENT ,TABORA

WAKUU wa Wilaya ya Tabora na Uyui wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi ili kuhakikisha wanaondoa matatizo mbalimbali katika maeneo yao ya utawala ili kuwasaidia wananchi kuwa na mazingira ya kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora baada ya kuwaapisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala na yule wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huo. Alisema wanatakiwa kuchapa kazi kwa bidii wakati wa kuwatumikia wananchi ili kuheshimu imani kuwa aliyowapa Rais ya kuwateua kuongoza maeneo hayo.

Mwanri alisema watakiwa kusimama katika nafasi zao kwa kutumia Sheria na taratibu zilizopo katika kukabiliana na matatizo kama vile mimba na ndoa za utotoni , utoro, uharibifu wa mazingira na uhalifu wa aina mbalimbali ili kuondoa mambo hayo ambayo yanakwamisha maendeleo ya Mkoa huo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwataka Wakuu hao wapya na wale waliopo kuhakikisha wanawahimiza wananchi Mkoani humo kukarabati na kujenga nyumba nzuri na za kisasa ili Mkoa huo nao uonekana kuwa wananchi wake wana makazi mazuri na sio kuendelea kukaa katika nyumba ambazo sio nzuri.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa neno la shukurani mada baada ya kuapishwa leo.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala akitoa neno la shukurani mada baada ya kuapishwa leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...