Na. Ofisa Habari Mufindi 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (OR-TAMISEMI) Mhe Joseph Kakunda, amesema serikali ipo katika hatua a mwisho kukamilisha mchakato wa kuajiri waalimu 2000 wa masomo ya sayansi ili kupunguza changamoto ya uchache wa walimu wa kada hiyo katika shule za umma nchini

Mhe. Kakunda ameyasema hayo katika shule kongwe ya Sekondari Mdabulo, akiwa kwenye ziara ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya Mkuu wa shule hiyo Bw. George Mgomba, kueleza changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi katika shule yake.

“Serikali kwa mwaka huu inaendelea na mchakato wa kuajiri walimu wa sayansi wapatao 2000 hivyo, taarifa yenu naichukua mwenyewe na kuipeleka kwa Mhe. Waziri Jafo, bila shaka walimu wawili 02 mnaowahitaji katika shule yenu mtawapata na hili nalibeba kwa ajili ya utekelezaji” alisisitiza Waziri Kakunda

Aidha, Mhe. Kakunda ameridhishwa na majengo mapya ya Shule hiyo iliyojengwa kwa mfumo wa “Force Account” kwa kuzingatia maelekezo ya kitaifa baada ya kujionea madarasa na mabweni mazuri hivyo, amesisitiza utaratibu uliotumika wa kujenga kwa njia ya Force Account uendeleee hata wakati wa mradi wa ujenzi wa mabweni utakapoanza, ambapo serikali tayari imetenga Jumla ya Tsh Milioni 100 kwa shule ya Sekondari Mdabulo.


Naibu waziri Kakunda, akiongozwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo kukagua madarasa na mabweni mapya yaliyojengwa SerikaliNaibu waziri Kakunda akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...