Na Chalila Kibuda.
Maamuzi yanapotakiwa kufanyika ni lazima uwepo ushirikishaji ili kuweza kuendesha taasisi na kupata mafanikio ya kimaendeleo na taifa kuona tija ya tasisi husika.
Hayo aliyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila wakati akifungua Baraza la Pili la Shirika la Taifa la Madini (Stamico) amesema sheria ya mashauriano katika utumishi wa umma, serikali imebainisha nia yake thabiti ya kutaka kuona wafanyakazi wakishirikishwa katika kusimamia na kuendesha taasisi wanazozimamia.
Amesema kuwa baraza ni chombo muhimu katika taasisi hivyo lazima kitumike katika kujadili mambo mbalimbali yanayoyohusu masilahi na ustawi wa watumishi , mipango na malengo ya kazi ya kuishauri menejimenti ya Stamico.Profesa Msanjila amesema viongozi waliochaguliwa katika baraza la wafanyakazi wa stamico kunadhihirisha imani ya wafanyakazi kuwa kile wanachokitaka kitafanyika kutokana na maamuzi ya ushirikishwaji.
Nae Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Stamico Mhandisi Kanali Sylvester Ghuliku amesema baraza lilopita lilikuwa na changamoto nyingi ambazo zilikuwa zinatokana na shirika lenyewe kwa kutokuwa na fedha za kuitisha mkutano wa baraza na fedha ambazo zilikuwa zinapatikana katika shirika kidogo na hata kuendesha ofisi hazikutosha.Amesema kuwa baraza litafanyaka kazi katika misingi iliyowekwa katika uanzishaji katika kufikia lengo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akizungumza na baraza jipya la wafanyakazi la pili la Stamico lilofanyika Ofisi za Stamico jijini Dar es Salaam.
Watoa maada kutoka ofisi ya Kamishina wa madini, , Idara ya kazi na wawakilishi kutoa Chama cha wafanyakazi wa Migodi, Nishati , Ujenzi na Kazi Nyinginezo (Tamico)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila wa sita kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la pili jipya la Wafanyakazi wa Stamico, kulia kwa katibu Mkuu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Stamico Mhandisi Kanali Sylvester Ghuliku wane kutoka kushoto mstari wa mbele ni Katibu Mpya wa Baraza hilo Juma Mbawambo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...