Na Asteria Muhozya, Simanjiro

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema Serikali itaaendelea kusimamia ulinzi na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao kinakuja.
Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani Manyara wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini ya tanzanite ndani ya ukuta wa Mirerani.

Alisema ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini mengine zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite unavyoendelea katika migodi husika. Kairuki aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga kuangalia namna Sheria ya Madini inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya watumishi katika migodi na namna migodi husika inavyolipa kodi mbalimbali za Serikali yakiwemo masuala ya usalama sehemu za kazi na wafanyakazi kwa ujumla.

“Utoroshaji madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania walio wengi kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo. Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,” alisema Kairuki.

Awali, akizungumza katika eneo Lemshuku kunakofanyika shughuli za uchimbaji wa madini ya Green Garnet, waziri Kairuki alisema kuwa, serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kuchangia pato la taifa kupitia shughuli za uchimbaji, hivyo akawaasa wachimbaji nchini kufuata Sheria, kanuni na taratibu ili kufanya shughuli halali ikiwemo kulipa kodi stahiki.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia moja ya seal inayotumika kufunga madini ya tanzanite baada ya kuzalishwa na kufanyiwa tathmini kwa lengo la kuhakikisha serikali inapata mapato yake stahiki.
Waziri wa Madini Angellaha Kairuki akipima ubora wa madini ya Tanzanite katika kifaa maalum baada ya kuzalishwa kutoka katika mgodi wa moja ya wachimbaji madini ya tanzanite.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia madini ya Green Garnet alipotembelea moja ya migodi inayochimba madini hayo katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara wakati wa zira yake.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akieleza jambo wakati akipata ufafanuzi kutoka kwa mchimbaji (aliye ndani ya shimo) wakati alipotembelea moja ya migodi ya madini ya Green Garnet katika eneo la Lemshuku wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara.
Sehemu ya wachimbaji katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro kunakofanyika shughuli za uchimbaji madini ya Green Garnet wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki hayupo pichani wakati wa ziara yake katika eneo hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...