Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini,
MADIWANI
wanne kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika
manispaa ya Moshi pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi wamejitokeza kumuunga mkono Diwani
wa kata ya Shirimatunda ,Francis Shio (Chadema) kuhamasisha uchangiaji
katika shughuli za maendeleo.
Madiwani
waliojitokea katika mkutano maalumu wa Diwani kata na wananchi wa kata
hiyo ,ni pamoja na Diwani wa kata ya Soweto,Collins Tamimu,Diwani wa
kata ya Njoro na Naibu Meya wa manispaa ya Moshi,Jomba Khoi ,Diwani wa
kata ya Ng’ambo Genesis Kiwhelu na Diwani wa kata ya Kiboriloni ,Frank
Kagoma.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya kata ya Shirimatunda
,Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Fransic Shio alisema maendeleo ya
wananchi katika maeneo yao yataletwa na wananchi wenyewe na si itikadi
za kisiasa kama baadhi ya wanasiasa wanavyoamini.
“Shirimatunda
yetu ni ya kwanza kuliko vitu vingine,haya ninayo yasema ni ya uwazi
tukikubali kuyaingiza mambo ya kisiasa katika maendeleo ya kata yetu
,yapo mambo mengi sana yatasimama ,ni lazima kaul yetu ya wana
Shirimatunda,umoja ya wana Shirimatunda na amani yetu tuweze kuilinda
kwa gharama yoyote”alisema Mh Shio.
Shio
aliwataka wakazi wa Shirimatunda kuwaondoa katika misingi ya umoja wa
wakazi wa kata ya Shirimatunda huku akiwaomba kupitishwa azimio la
kuchangisha fedha kwa kila familia katika kata hiyo kutoa kiasi cha Sh
10000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa la wanafunzi wa shule ya awali.
Kwa
upande wao ,Madiwani waliofika kumuunga mkono Diwani huyo,walisema ili
kushawishi wadau mbalimbali pamoja na serikali kujitokeza kuchangia
maendeleo katika kata hiyo wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa wa kwanza
katika kuchangia.
“Mgeni
akija nyumbani akakuta wewe mwenyewe hujielewi ,hata kama amekuja na
zawadi atarudi nayo ,watu wa Shirimatunda wanaangaliana nani anatoa nini
,endapo kila mkazi wa Shirimatunda akiguswa na hiki tunachokifanya basi
angechangia katika eneo hili la elimu”alisema Diwani Kagoma.

Diwani wa kata ya Shirimatunda katika Manispaa ya Moshi,Fransic Shio (CHADEMA) akizungumza wakati wamkutano wa kata uliolenga kujadili masuala ya maendeleo pamoja na kutambulisha wajumbe wanaounda kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza katika mkutano wa kata ya Shiriamtunda ambapo yeye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi .
Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro,Jomba Khoi akizungumza katika mkutano huo ambapo yeye na madiwani wenzake walifika kumuunga mkono Diwani wa kata hiyo katika kuchangia shuhghuli za maendeleo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...