Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema Serikali inaratibu vyema upatikanaji vibali vya kuagiza nyavu bora kwa ajili ya shughuli za uvuvi.
Ulega ametoa kauli jana katika mkutano wa hadhara na wakazi wa kisiwa cha Gana kilichopo wilayani Ukerewe alipofanya ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za uvuvi.
Ulega ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga amewaeleza wanakisiwa hao wa Gana kuwa Serikali imeshaanza kutoa vibali vya kuagiza nyavu kwa utaratibu unaofaa.
Wakazi hao walitumia fursa hiyo kumuuliza Ulega kuhusu hatima ya samaki aina ya Furu, Gogogo, Nembe na Ningu ambao hawatajwi na sheria ya uvuvi.
Ulega amewajibu "Serikali inaanda muongozo utakaowasaidia kuvua samaki hawa kwa uhuru " amesema .Pia amewataka wavuvi wa Gana wajiunge kwenye vikundi vya ushirika ili wapekelekewa mradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) wa wavuvi skimu.
"Mradi huu utakaokopesha na utawasaidia kuimarisha shughuli zao kupitia vikundi watakavyoviunda,"amesema Ulega.

Pichani kati ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega
akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa chama cha CCM,Ulinzi na usalama
wilaya,wakienda kwenye mkutano mara baada ya kuwasili katika kisiwa cha
Ghana wilayani Ukerewe
Pichani
kati ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiwa
sambamba na baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wilaya,wakiwa ndani
ya boti kueleka kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe kukutana na wananchi
wakiwemo wavuvi katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero zao

Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa
kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe katika mkutano wa hadhara,alipofanya
ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za Wavuvi
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiagana na baadhi
ya viongozi (hawapo pichani),wakati akipanda boti kuelekea kisiwa cha
Ghana wilayani Ukerewe kukutana na wananchi wakiwemo wavuvi katika ziara
yake ya kutembelea na kusikiliza kero za Wavuvi hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...