Kwa kipindi cha miaka 10, maonyesho ya mavazi ya Swahili Fashion Week yamebaki kuwa mbele katika kutoa na kuwatengenezea njia wabunifu chipukizi katika tasnia ya mitindo Afrika mashariki na kati. Swahili fashion week kupitia shindano la kutafuta mbunifu chipukizi lijulikanalo kama Washington Benbella Emerging Designer Competition (WB-EDC) limekuwa likisherehekea vipaji vingi vya mitindo mbalimbali barani afrika na vile vile wabunifu chipukizi wamekuwa wakipata kujiamini na kuweza kuanzisha bidhaa zao.
Mwaka huu, katika mashindano haya yakiwa na dhima kuu ya “kukuza lugha ya Kiswahili” yamefungua rasmi milango kwa wabunifu vijana barani afrika kutuma maombi kwa fursa hii ya kipekee itakayo mpa nafasi ya kutambulika katika tasni ya mitindo na kupata uzoefu.
“tunafurahi fungua awamu ya 11 ya mashindano haya, na siku zote huwa tuna furaha ya kutoa fursa za thamani kwa wabunifu chipukizi wenye vipaji na hamasa ambao watawakilisha tasnia ya mitindo barani afrika kwa miaka ijayo. Hivyo tunawasihi wabunifu wote chipukizi kuikumbatia fursa hii kwa umakini na kutuma maombi kabla ya tarehe 30 Septemba 2018 saa 12 jioni.” Alisema Afisa uhusiano wa Swahili Fashion Week, Maryam Idriss.
Chipukizi 10 watakaochaguliwa kuingia fainali, watapewa nafasi ya kuonyesha mitindo ya nguo zao katika siku ya pili ya maonyesho ya Swahili Fashion Week ambayo itakuwa ni tarehe 1 Disemba 2018, kasha majaji watachagua mshindi na atazawadia tuzo na nafasi ya kushiriki na kuonyesha mavazi yake mengi zaidi katika maonyesho ya 12 ya Swahili Fashion Week mwaka 2019.
Fomu za maombi tayari zipo kwenye tovuti www.swahilifashionweek.com, tarehe ya mwisho wa kuwasilisha fomu ni 30 Septemba 2018 saa 12 za EAT. Waombaji wanakumbushwa kusoma maelekezo kwa makini ili wawasilishe maombi kamili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...