KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) ni mojawapo ya taasisi za Serikali zinazoshiriki kwenye Maonesho ya 25 ya Nanenane ambayo yameanza kufanyika nchini kuanzia Agosti 1 mwaka huu na yanatarajiwa kumalizika Agosti 11 huku TIC ikitumia nafasi hiyo kuelezea majukumu yake.

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda.Ili kuhakikisha taarifa na huduma kwa wawekezaji zinawafikia wadau wao kwa wigo mpana Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe amefanikisha kituo kushiriki kwenye maonesho katika mikoa mbalimbali nchini kupitia ofisi zao za Kanda.

Akizungumzia maoesho hayo Mwambe amesema lengo la kushiriki ni kutoa elimu kwa umma kuhusu taasisi yao, kazi wanazozifanya, huduma wanazozitoa kwa wawekezaji na taratibu zinazohitajika ili wadau (wazawa na wageni au ubia) waweze kujisajili na Kituo.

Hivyo Mwambe, anafafanua kuwa TIC inapatikana kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane nchini ambapo amesema wanashiriki katika Mkoa wa Simiyu(viwanja wa Nyakibindi) na Mbeya(viwanja vya Nanenane).

Pia mkoani Arusha(viwanja vya Njiro), Lindi (Ngongo),Tabora(Ipuli), Morogoro (Nanenane) na Dodoma(Nzuguni). Hivyo Mwambe ametoa mwito kwa umma na wadau kutoka mikoa ambapo maonesho yanafanyika na kutoka Mikoa jirani kutembelea mabanda ya TIC yanayopatikana katika maonesho hayo.

"Lengo ni kuwawezesha kupata taarifa na huduma za uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na namna ambavyo wawekezaji wazawa na wageni wanavyonufaika na huduma za Kituo."Kwa ujumla TIC inatumia maonesho ya Nanenane ili kuutarifu umma kuwa TIC inatoa huduma kwa wawekezaji wazawa na wageni kupitia ofisi zetu za Kanda ambazo zinapatikana katika Mikoa ya Mwanza, Moshi, Mtwara, Kigoma, Dodoma, Mbeya na Dar es Salaam,"amesema.Kusoma zaidi BOFYA HAPA>>>
 Afisa Habari wa TIC,Latiffa kigoda  akitoa maelekezo kwa wadau waliotembelea banda la TIC  Kanda ya Ziwa
 Bw. Venance Mashiba wa Kanda ya Mashariki akitoa maelekezo kwa washiriki wa nane nane yanayofanyika Mkoani Morogoro
 Afisa Uhamasishaji Uwekezaji , Bw. Sindano Ajelandro akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea banda la TIC  88 Mkoani Mbeya
 Bw. Fanuel Lukwaro Meneja wa TIC Kanda ya Ziwa akisikiliza kwa makini hoja za mdau alipotembelea banda la TIC 88 Mkoani Simiyu
Bw.Doto Stanley Meneja Kanda ya Kusini akishiriki 88 Mkoani Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...