Na.Vero Ignatus -Arusha
Tume
ya Nguvu za Atomiki Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa wakulima na
wafugaji juu ya uthibiti wa viasilia vya mionzi vinavyoweza kupatikana
kwenye mazao ya chakula na mifugo ili kuongeza usalama wa mtumiaji dhidi
ya madhara hatari yanayosababishwa na mionzi.
Katika
maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini wanatoa elimu juu ya nyuklia
inayoweza kuwa mkombozi kwenye ukuaji wa uchumi wa biashara na viwanda
ikilenga matumizi salama teknolojia nchini ili kuboresha ustawi wa
kwenye sekta ya afya,maji ,kilimo,nishati na mifugo.
Mtafiti
wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Yesaya Sungita amesema takwimu zinaonyesha
kwamba zaidi ya asilimia 30%ya vyakula duniani vinahribika kila mwaka
kwa sababu ya kuharibiwa na na vijidudu au kuoza ,upotevu au kuharibika
kwa chakula kuna athari kubwa katika kipato cha wakulima.
Aidha
kila mwaka inakadiriwa hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya
nafaka barani Afrika haswa kusini mwa jingo la sahara inafikia dola za
kimarekani bilioni 4 sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno
hayosambamba na matukio ya binadamu kuambukizwa vijidudu vya salmonella
yanafikia iddi ya watu 120,000 kila mwaka ambapo maambukizi yamekuwa
yakisbabisha vifo vingi.
"Gharama
ya matibabu yanayosababishwa na madhara ya maambukizi haya ya vijidudu
vya salmonella na Ecoli yamekuwa yakisababisha hasara ya dola za
kimarekani bilioni 6 kila mwaka.alisema Yesaya"
Kutoka kulia ni Mtafiti kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Yesaye Sungita, wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Tume Peter Ngamilo akiguatiwa na Mtafiti wa Tume hiyo Jerome Mwimanzi wakitoa elimu kwa mmoja wa mgeni aliyetembelea katika banda hilo katika maonyesho ya nane nane Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...