Na.khadija Seif,Globu ya jamii

Muandaaji wa kinyang'anyiro cha Wanamitindo nchini ambae pia alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998, Basilla mwanukuzi amezungumza jijini Dar es salaam na wanahabari kuhusu hafla ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia kilele septemba 8 mwaka huu katika ukumbi  wa Julius Nyerere international convention Centre (JNICC).

Aidha Mwanukuzi ametoa shukrani kwa Waziri wa Sanaa,utamaduni na michezo Mh.Harrison Mwakyembe kwa kushirikiana na mashindano hayo tangu yalipoanza mchakato wake  April mwaka huu, na kufungua rasmi kwani kulikuepo na changamoto mbalimbali hapo awali likiwemo suala la kufungia mashindano hayo kutokana na sababu mbalimbali, ambapo kimsingi ziliwanyima warembo wengi fursa ya kushiriki.

"Hivyo basi kwa sasa wamepatiwa fursa hiyo na tunategemea tutapata mshindi ambae ataipeperusha bendera yetu Kwenye mashindano ya miss World ambayo yatafanyika nchini China ",alieleza Basilla.Pia ametolea ufafanuzi kuhusu vigezo ambavo vimewekwa bayana kwa mrembo atakaeshinda taji hilo, ikiwemo umri pamoja na uraia wa Tanzania sambamba ukiwekwa mbele zaidi .

Mshindi wa miss Tanzania atapatiwa taji lenye thamani ya shilingi za kitanzania millioni 6 pamoja na gari lenye hadhi nzuri na viwango pamoja na kupata fursa ya kusaidia jamii yake.
Muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania Basilla Mwanukuzi akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu mashindano ya warembo hao yanayotarijiwa kufikia kilele chake mwanzoni mwa septemba mwaka huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...