Ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara, mchana wa leo.
Marehemu Sagati alifariki dunia pamoja na watu wengine wawili katika ajali wilayani Geita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema ajali hiyo ilitokea Jumatatu Septemba 30, 2018 wakati dereva wa gari lenye namba STK 9565 aina ya Toyota Land Cruiser V8, alipomkwepa mpita njia, Happiness James (7), aliyekatiza barabarani ghafla wilayani Chato, Mkoa wa Geita.
Alisema kutokana na ajali hiyo, watumishi wa wizara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Ludovick Nuhiye, Mchumi Nickson Matembo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Yusuph Mbwalwa na dereva, Lucas wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita wakipatiwa matibabu.
Kamanda Mwabulambo alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Minkoto, Kijiji cha Kalembela wilayani Chato mkoani Geita. “Gari hilo lilikuwa likitokea Mkoa wa Kagera kwenda Mwanza na binti huyo alinusurika kugongwa baada ya dereva kufanya jitihada za kumkwepa.
“Dereva alilazimika kupeleka gari upande wa kulia ambako pia alikutana na kumgonga na mpitanjia, Semeni Kibiriti, ambaye alifariki dunia hapo hapo.
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa MaraKiongozi wa dini akiongoza ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
Ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikiendelea nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
Wanahabari Mgaya Kingoba na Abdulwakil Saiboko wakisaidiana na waombelezaji wengine kuweka sawa jeneza wakati wa ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
Sehemu ya waombolezaji katika ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara
Viongozi wa dini wakiongoza ibada ya mazishi ya mwanahabari Marehemu Shadrack Sagati ikifanyika nyumbani kwao kijiji cha Mwiruruma, wilayani Bunda, mkoa wa Mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...