Zuhura (Venus), Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturn) na Mirihi (Mars) zinaonekana angani zikiwa katika mstari mnyoofu kutoka magharibi kwenda mashariki na Mwezi unazikaribia kati ya tarehe 14 hadi 23 Agosti, 2018.

Muda wa kuziona sayari zote hizi ni kuanzia saa moja. Zuhura itatua magharibi na kupotea baada ya saa tatu.

Sayari huonekana kama nyota angani kwa hiyo namna ya kutofauitsha ni kwa mn'gao wake. Sayari ya Zuhura (Venus) inawaka kabisa kwa unjano upande wa magharibi wakati Mirihi (Mars) inamulika kwa rangi nyekundu upande wa mashariki.

Mshtarii (Jupiter) inan'gaa sana utosini.

Mn'gao wa Zohali (Saturn) ni mkali lakini ni sawa na nyota zingine. Kwa hiyo namna ya kutofautisha ni kwamba mwanga wa sayari zote haumeremeti kama nyota za kawaida.

Kwa hiyo ukiangalia nyota kwa makini na kama haimeremeti basi ni sayari. Imeandaliwa na Dkt. Noorali T. Jiwaji 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...