Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIKAMOO Mheshimiwa Rais Dk.John Magufuli.
Pia naomba kutumia nafasi hii kutoa pole nyingi kwako kutokana na msiba wa kuondokewa na dada yako mpendwa Monica Magufuli.

Pole Rais wangu, pole familia ya Rais, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu aiweke roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi. Amina. 

Baada ya utangulizi huo naomba niseme jambo kidogo. Nilishiriki uchaguzi Mkuu mwaka 2015 na kura yangu ya Urais nilikuchagua wewe.

Nikiri sikukosea kwa uamuzi wa kura yangu kukupa wewe uwe Rais wangu. Sijakosea na nashukuru Mungu alinipa utulivu wa kuchagua Rais sahihi kwa ajili ya maisha ya Watanzania wote.

Rais wangu mpendwa nimekuwa nikifuatilia utendaji wako wa kazi, nimekuwa nikifuatilia maagizo yako kwa walio chini yako.Kubwa zaidi nimekuwa nikifuatilia hotuba zako mbalimbali.

Naomba nikiri Rais wangu hotuba yako ambayo umeizungumza wilayani Chato imenigusa mno. Najua umetoa hotuba kadhaa ukiwa Chato lakini naomba nikukumbushe naizungumzia hii hotuba yako ya  kuhusu makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Hotuba yako imethibitisha namna ambavyo unaamini katika kusimamia misingi ya utawala wa sheria.

Najua namna ambavyo umewakosha wengi. Umewakosha si kwa sababu wanamchukia au wanampenda saana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, bali ni kwa kuonesha unavyosimamia sheria.

Ujue Rais wangu huku mtaani ninakoishi kuna mengi yamekuwa yakizungumzwa. Wapo wanaosema unampenda sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sababu unampenda basi hata akikosea huwezi kumchukulia hatua.

Si mimi ninayesema, ila huku mtaani ndio wanavyosema hivyo. Ukweli ni kwamba mtaani kuna maneno maneno mengi yanazungumzwa hasa tukiwa kwenye vijiwe vya kahawa. Basi bwana watu wanazungumza lakini wakifika kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam utasikia wakisema “Huyooo RC wa Dar anapendwa sana. Hawezi kuchukuliwa hatua.”
Napokea maoni kwa 0713 833822.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...