Na Gaudensia
Simwanza – Urambo.
TFDA
kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wanaendesha mafunzo
ya siku tano kwa wajasiriamali wadogo 150 wa usindikaji wa vyakula wilayani
humo kuanzia leo tarehe 20/8/2018 ili
kuchangia ukuaji wa Sekta ya viwanda
nchini sanjari na kuinua uchumi wa wananchi wa Urambo.
Mafunzo
hayo yamefunguliwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Angelina
Kwingwa na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa Wilaya hiyo wakiwemo Mbunge, Mhe. Margareth Sitta (Mb.), Katibu wa CCM wa
wilaya, Bi. Jesca Mbogo na Mkurugenzi wa wilaya, Bi. Margareth Nakainga
miongoni mwa viongozi wengine.
”TFDA inatambua mchango mlio nao katika
kukuza viwanda vidogo vya chakula kwani kutokana na uwingi wake vina mchango
mkubwa katika; kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha
mazao ya chakula na kuyasindika na hatimaye kuiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025”, alisisitiza Mgeni Rasmi huyo.
“Ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo
nchini kutatua changamoto zinazowakabili katika usajili wa majengo na bidhaa zao,
uongozi wa Wilaya umeamua kuweka mkakati wa makusudi ikiwa ni pamoja na
kuwaalika wataalam wa Serikali kuja kutoa mafunzo kama haya ili kuinua maisha
ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla”, Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza.
TFDA inaendelea kushirikiana uongozi wa Mikoa na Halmashauri zake ili
kuwawezesha Watanzania kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwa
kuzingatia vigezo vya usalama na ubora ili kupata soko la ndani na nje ya nchi
kwa bidhaa zetu kwa maendeleo ya Taifa

Mgeni
Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Angelina Kwingwa, (aliyesimama) akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo yanayoendeshwa na TFDA kwa Wajasiriamali wa
Wilaya ya Urambo. Viongozi wengine wa wilaya hiyo kutoka kushoto ni Mbunge wa
wilaya Mhe. Margareth Sitta (wa tano), Mkurugenzi wa wilaya, Bi. Margareth
Nakainga (wa sita), Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa
saba), Katibu wa (CCM) wa wilaya, Bi. Jesca Mbogo (wa tatu), na Mwenyekiti wa
semina hiyo, Bi. Martha Susu (wa n ne).
Mbunge
wa wilaya ya Urambo Mhe. Margareth Sitta (aliyesimama), akiwasalimia
wajasiriamali wanaohudhuria mafunzo wilayani Urambo.
Sehemu
ya Wajasiriamali wilaya ya Urambo
wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na (TFDA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...