Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Kebwe Steven Kebwe akisalimiana na
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay
alipofika ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huyo hivi karibuni mjini Morogoro.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni mstaafu John
Chiligati, Mtendaji Mkuu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe na mmoja wa
wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Bw. Emmanuel Mayeji.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Cliford Tandari akiteta jambo na
wajumbe Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) pamoja na watendaji wa mpango
huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Daniel Ole Njolay
(katikati) walipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro hivi
karibuni. Kutoka kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Emmanuel Mayeji,
Mtendaji Mkuu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe, Mwenyekiti mstaafu wa
kamati hiyo Kapteni John Chiligati na mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo,
Bw. Ibrahim Janabi.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogorgo, Bi. Ruth John akielezea jambo
mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) pamoja na
watendaji wa mpango huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi
Daniel Ole Njolay (katikati) walipotembelea ofisi za Mkuu wa Wilaya ya
Morogoro hivi karibuni.
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Bibi. Anna Mwasha aakifafanua
jambo mbele ya Afisa Biashara wa Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni
Mratibu wa MKURABITA katika Manispaa hiyo, Bw. Herman Festus wakati wa
ziara ya kutembelea Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa
Biashara katika Manispaa ya Morogoro hivi karibuni.Kituo hicho kinatoa
huduma za urasimishaji wa biashara ambapo mpaka sasa kimefanikiwa
kurasimisha biashara 5000 na kufanyikisha ukusanyaji wa mapato ya
takribani shilingi milioni 500. Kulia kwake ni Meneja wa Urasimishaji wa
Biashara Heavy Kombe na mmoja wa watoa huduma wa Kituo hicho Bi. Mary
Lyimo.
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA),Bibi. Seraphia Mgembe akijadili jambo na
Mwenyekiti wa Kampuni ya Wanawake Wazalishaji wa Chakula Tanzania
(WFPT), Bibi. Emmy Kiula hivi karibuni mjini Morogoro. Kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay.
Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA),Bibi. Seraphia Mgembe akikagua kifungashio
cha mvinyo walipotembelea Kampuni ya ADUKE Food Processing wakati wa wa
ziara ya kutembelea wanufaika wa mafunzo ya MKURABITA mkoani Morogorogo
hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA),
Balozi Daniel Ole Njolay, kushoto ni Afisa Biashara Manispaa ya
Morogoro, Herman Festus na wapili kushoto ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi
ya MKURABITA Bibi. Angelista Kihaga.
Mwenyekit wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay akiongoza kikao cha majumuisho baada ya kuhitimisha ziara ya siku 12 kukagua maendeleo ya utekelezaji ya shughuli za Urasimishaji Ardhi na Biashara katika maeneo ya Urambo, Bariadi, Ikungi, Chamwino na Manispaa ya Morogoro kikoao kilichofanyika mjini Morogoro mapema hivi karibuni. Picha na Frank Shija- MAELEZO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...