NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na taasisi ya WEPMO (Water and Environmental Sanitation Projects Maintanance Organisation) imewahimiza wananchi kujenga vyoo bora kwani inaonyesha kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa vyenye kutumia maji na sakafu inayosafishika ni asilimia 50 pekee.

Pande hizo zipo katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa afya na usafi wa mazingira kwa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu akizungumza katika utambulisho wa mradi huo utakaotekelezwa kupitia kampeni ya “Usichukulie Poa nyumba ni Choo” alisema, halmashauri imekuwa ikifanya uhamasishaji huo kupitia maafisa afya wa kata kila mara.

"Mradi huu unatekelezwa katika kata zote 11 za halmashauri ambapo wananchi wanahamasishwa kujenga vyoo bora kwa bei nafuu na kuelimishwa juu ya umuhimu wa kila nyumba kuwa na choo bora" alisema Fatuma.Fatuma aliiwashukuru taasisi ya WEPMO kwa kuja kuongeza nguvu katika uhamasishaji huu wa ujenzi wa vyoo bora.

Alielezea “Ni lazima kila mmoja afanye wajibu wake, wataalam wawajengee wananchi uelewa juu ya ujenzi na utumiaji wa vyoo bora""Ni vyema wananchi wakaelewa kwanza kabla watendaji wa kata hawajatumia nguvu na sheria kwa watakaokaidi kujenga na kutumia vyoo bora katika kaya zao kwa kuwafungulia mashauri katika mabaraza ya kata”alisisitiza.

Nae mratibu wa mradi huu wa uboreshaji wa afya na usafi wa mazingira katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Renatus Rweyemamu alisema katika utafiti wa awali uliofanywa na taasisi hiyo, hali ya afya na usafi wa mazingira inaonesha asilimia 84 pekee ndio wananchi wenye kaya zenye vyoo vya kawaida.Alisema , yaani aina yoyote ya choo kinachotenganisha kinyesi na mazingira hata vile visivyosafishika, ilihali, kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa vyenye kutumia maji na vyenye sakafu inayosafishika ni 50% .Rweyemamu alielezea , vyoo vyenye vifaa vya kunawia mikono zikiwa ni asilimia 18 pekee. 

Alifafanua ,lengo la mradi huo ni kuongeza ufahamu kwa wananchi kutambua athari za kujisaidia ovyo katika mazingira .
Mratibu wa mradi wa Uboreshaji sekta ya Afya na usafi wa mazingira H/W Bagamoyo Renatus Rweyemamu akitoa maelezo ya mradi kwa wataalm wa halmashauri.( picha na Mwamvua Mwinyi)
Afisa Afya Wilaya ya bagamoyo Bi. Joyce Nganzo akichangia mada wakati wa utambulisho wa mradi wa uboreshaji sekta ya Afya na Usafi wa mazingira Bagamoyo.
1. Picha ya pamoja ya wataalamu wa Halmashauri, Watendaji wa kata za bagamoyo na wataalamu wa Taasisi ya WEPMO mara baada ya utambulisho wa mradi wa uboreshaji sekta ya Afya na usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya bagamoyo.( picha na Mwamvua Mwinyi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...