Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Timu ya riadha ya Polisi imeagwa jana mchana na kuondoka leo kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO GAMES).
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Yusuf Ilembo aliwataka askari hao kutanguliza uzalendo kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla hivyo wajitume kwa uwezo wao wote ili waweze kuibuka na ushindi mnono.
“Ingawa tuna wawakilishi katika michezo mbalimbali lakini Jeshi la Polisi lina mategemeo makubwa juu ya mchezo wa riadha hivyo naimani mtachukua medali zote na hatimaye kuwa washindi”. Alisema Afisa Mnadhimu huyo.
Wanariadha hao Kumi na Nane walioweka kambi kwa muda wa miezi sita eneo la Ilboru wilaya ya Arumeru watashiriki Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza tarehe 06 Agosti jijini Dar es saalam kwa kukimbia mbio ndefu na mbio za kati.
Akizungumzia maandalizi ya kambi hiyo, Msimamizi wa Michezo toka Shule ya Mafunzo ya Polisi Moshi, Inspekta Emmanuel Mtatifikolo alisema wana matumaini makubwa ya kushinda nafasi za juu na hawataliangusha Jeshi la Polisi japokuwa kuna nchi tishio kama vile Kenya na Uganda.
Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Yusuf Ilembo akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha hao pamoja na viongozi wa Polisi ngazi ya mkoa 
(Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...