Na Oliver Njunwa 

Wapelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki wametakiwa kuharakisha mchakato wa kuandaa mtaala wa kuwajengea uwezo wapelelezi wa kodi pamoja na mfumo wa kisheria ili kuweza kushirikiana katika kupambana na uhalifu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wito huo umetolewa na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi wakati akifungua Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar.

“Tunataka mchakato huu umalizike mapema ili tuweze kupambana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi kwani kadri tunavyochelewa ndivyo na wahalifu wanaendelea kusababisha upotevu wa kodi kwa mamlaka zetu za mapato”, alisema Bw. Kessi.

Aliongeza kwamba kwa siku nne ambazo watakuwa Zanzibar wanatakiwa kukamilisha hiyo kazi ili iweze kuwasilishwa katika kikao cha Makamishna wa Upelelezi wa Kodi Afrika Mashariki ambao walikubaliana kushirikiana kufanya upelelezi wa kodi kwa pamoja kupampana na kudhibiti uhalifu katika masuala ya kodi.
Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki. 
Wajumbe wa Kamati ya wapelelezi wa kodi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (hayupo katika picha) wakati akifungua rasmi mkutano. 
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki katika picha ya Pamoja na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (katikati walioketi) mara baada ya ufunguzi wa mkutano katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...