Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Watu 11 wakiwamo raia wawili wa Guinea wamepandishwa katika Kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kukutwa na vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.5.

Mapema leo asubuhi washtakiwa hao waliachiwa na kufunguliwa mashtaka mapya baada ya masaa matatu yale yale. Awali walikuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo hayo ya uhujumu uchumi ambapo waliachiwa huru na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde lakini baada ya kuachiwa walikamatwa na ndani ya Masaa matatu walipandishwa tena kizimbani na kusomewa mashtaka mapya.
Wakiwasomewa mashtaka mapya mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizire, Wakili wa Serikali, Salim Msemo amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ally Shariff na Fatoumata Saumaolo raia wa Guinea, Victor Mawalla, Calist Mawalla, Solomoni Kuhembe, Haruna Abdallah’ Kasa’, Abas Hassan ‘Jabu’,Ismail Kasa, Khalfan Kahengela, Musa Ligagabile na Kassim Said@ Bedui.
Imedaiwa kuwa washtakiwa kwa pamoja kati ya Aprili 6 na Juni 23, 2016 jijini Dar es Salaam, waliratibu na kusafirisha vipande 660 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 2,105, 181 ambazo sawa na biklioni 4.5 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na sheria ya wanyama pori.

Imedaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao walijihusisha na nyara za Serikali kinyume na sheria ya wanyamapori ambapo wanadaiwa walisafirisha vipande hivyo.Pia washtakiwa watano kati ya hao, Ally, Victor, Calist,Haruna na Abbaswanadaiwa kuwa walikutwa na vipande vya meno ya tembo kinyume na sheria za wanyamapori.
Hata hivyo, Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea.

Hata hivyo washtakiwa hao walilalamika mahakamani hapo kuwa hiyo siyo kesi mpya ilifutwa Masaa matatu kabla hawajafunguliwa kesi hiyo mpya hivyo waliomba kutendewa haki kwa sababu wanaumia gerezani na upande wa mashtaka unaumiza familia zao.Hivyo waliomba hiyo kesi iende mahakama Kuu kwa sababu hapo hawawezi kupata haki.
Wapo ndani tangu mwaka 2016 wakitaka kuomba dhamana mahakama Kuu Upande wa Mashtaka unawaeleza kesi imeiva, wahisi wanataka kuwauwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 3,2018.
  Watuhumiwa 11 wa kesi ya Uhujumu Uchumi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...