Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) utafanyika Beijing kuanzia tarehe 01 hadi 04 Septemba, 2018.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Viongozi wengine watakaoshiriki Mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga; Mhe. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Viongozi wengine Waandamizi.
Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa China, Mhe. Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti wa jukwaa hilo, kwa kushirikiana na Mwenyekiti Mwenza, Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa, utahudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika ambaye pia ni Rais wa Chad, Mhe. Moussa Faki Mahamat. Mkutano huo pia utashuhudia uchaguzi wa Mwenyekiti Mwenza mpya kutoka Afrika.
Kaulimbiu ya Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mwaka 2018 ni “China na Afrika: Kuelekea Jumuiya Imara kwa mustakabali wa wote kupitia ushirikiano kwa manufaa ya wote” (China and Africa: Toward an Even Stronger Community with a Shared Future through Win-Win Co-operation).
Kusoma zaidi bofya hapa.
Kusoma zaidi bofya hapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...