Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa wana mikakati ua kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu ili kuweza kupata nafasi ya kucheza tena michuano ya Kimataifa kwa kuchukua ubingwa msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JKNIA Mwenyekiti wa Mashindano Hussein Nyika amesema kuwa kwa wamejiwekea mikakati mipya ya kuweza kuona wanafanya vizuri ikiwemo kupata ushindi katika kila mchezo ili wapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Nyika amesema kuwa ratiba yao ilikuwa ni kucheza na Mwadui ila kwa kuwa ratiba ya ligi imesimama  wanasubiri maamuzi ya mwalimu kuona wanaendelea na mazoezi ambapo wachezaji walioitwa na timu ya Taifa watajumuika kambini ila hawa ambao hawajaitwa watapewa mapumziko ya siku moja.
Amesema kuwa, baada ya kuhairishwa kwa mechi yao hiyo dhidi ya Mwadui kulikuwa na ratiba ya mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United uliokuwa ufanyike mkoani Kigoma ila mpaka sasa hawajapata maamuzi ya mwalimu.

Nyika amesema kuwa hawajarejea na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kwasababu amekuwa na majukumu ya kitaifa akiwa kama Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC na atarejea pindi pale atakapokamilisha majukumu yake.
Akijibu swali huku mchezaji Feisal Salum kuondolewa katika timu ya Taifa, Nyika amesema kuwa yeye ndo amerejea nchini kwa sasa na hajapata taarifa hizo hawezi kujibu lolote na kusema hawezi kufanya kazi kwa kusoma kwenye mitandao ya kijamii.
Yanga imerejea nchini Leo baada ya kukamilisha ratiba ya Kombe la Shirikisho katika hatua ya makundi baada ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya Rayon Sports ya nchini Rwanda na kushika nafasi ya mwisho wakiwa na alama 4 huku Rayon na USM Alger wakifanikiwa kutinga hatua ya robo  fainali.
Kikosi cha Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...