SEKTA ya kilimo ni mhimili wa uchumi wa Taifa na inategemewa katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025, kupitia viwanda kwa sababu kilimo ndicho kitawezesha viwanda kwa kuvipatia malighafi.

Kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa nchini, serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhakikisha inaiboresha ili iweze kuwa na tija na kufikia malengo iliyojiwekea.

Sekta hiyo mbali na kuwa mhimili wa uchumi wa Taifa, pia imekuwa ikichangia pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za kigeni.Kufuatia hali hiyo, Serikali imeweka msisitizo katika kusimamia mazao makuu matato ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku ambayo uzalishaji wake umeonyesha tija.

Baada ya kupata mafanikio katika mazao hayo Serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha mazao ya alizeti, ufuta, michikichi ili kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa kutumia mazao hayo na mbegu za pamba.Itakumbukwa kwamba kila mwaka, Serikali inatumia sh. bilioni 600 kwa ajili ya kuagiza mafuta ghafi ya kula kutoka nje ili kukidhi mahitaji kwa kuwa kiwango kinachozalishwa nchini hakitoshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...