Katika kuwajengea Watanzania mazingira salama na rahisi ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao, Jumia
imesisitiza kuwa bidhaa zote zinazopatikana kwenye mtandao wake ni
halisi na zenye bora wa hali ya juu kutoka kwa kampuni na
wafanyabiashara wanaoaminika Tanzania na duniani kote.
Kwa watanzania wengi dhana ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao bado ni ngeni na haijazoeleka. Miongoni mwa sababu zinazopelekea hali hiyo ni; uaminifu kwa sababu hakuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya muuzaji na mnunuzi, hofu ya wizi wa mitandaoni kutokana na upya wa huduma hii pamoja na changamoto ya maendeleo ya kiteknolojia ambayo watu wengi bado hawajafikiwa nayo.
Watanzania wengi wamezoea kwenda maduka moja kwa moja pale wanapohitaji kununua bidhaa kwa sababu hupata wasaa wa kuziona, kuzishika, kuzijaribisha, kufanya makubaliano ya bei ili kujiridhisha zaidi kabla ya kukata shauri la kununua.
Akizungumzia juu ya faida ambazo zimeletwa na mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao kwa wafanyabiashara na wateja wa Kitanzania, Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, kampuni inayoongoza kwa huduma za manunuzi mtandaoni Afrika, Bw. Albany James amebainisha kuwa mfumo huu upo kwa ajili ya kuwarahisishia wateja huduma za kufanya manunuzi pamoja na kuongeza thamani kwa wafanyabiashara.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...