Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Dkt. Alex Mubiru ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.

Makamu wa Rais amesema kuwa AfDB imeahidi kuendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania kutokana na hatua kubwa ya kimaendeleo ambayo nchi yetu imeonyesha.Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika alisema kuwa wapo hapa kusaidia Serikali ya Tanzania pamoja na Watu wake.

Wakati huo huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Kenya nchi Mhe. Dan Kazungu ambaye alifika Ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.Mwisho Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida ambaye amemaliza muda wake hapa nchi.

Makamu wa Rais alimshukuru Balozi Yoshida kwa ushirikiano wote alioutoa kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.Nae Balozi Yoshida aliishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na watu wake kwa Ushirikiano mzuri waliompa  kwa kipindi chake alichohudumu kama Balozi wa Japan hapa nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake nchini Mhe. Masaharu Yoshida aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Rais leo Ikulu jijini Dar es Salaam kuaga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha leo Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha leo Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha ya Mwanamke shujaa katika Historia ya Kenya aliyefahamika kwa jina la Mekatilili Wa Menza kutoka kwa Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...