Waziri
wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki (wa
tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (katikati)
pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki
ya CBA Tanzania, Julius Konyani (wa pili kushoto) wakiungana na watu
wengine kumsikiliza Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya
Same, Entuja Mbwambo wakati akionyesha namna ya kutumia mashine maalum
ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati (Njiti) kupumua
vilivyotolewa na Benki ya CBA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya
Doris Mollel kwa hospitali hiyo, ambavyo thamani yake ni zaidi ya
shilingi 20 milioni.
Waziri
wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki pamoja
na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki ya CBA
Tanzania, Julius Konyani wakishirikiana kupanda mti katika eneo la
Hospitali ya Wilaya ya Same, muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa tiba
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 20 milioni, vilivyotolewa na Benki
ya CBA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kwa
hospitali hiyo kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
(Njiti).
Waziri
wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki
pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki
ya CBA Tanzania, Julius Konyani wakimsikiliza Mganga Mkuu wa wilaya ya
Same, Dkt Godfrey Andrew wakati akifafanua jambo kuhusu vifaa vita
alivyovipokea Hispitalini hapo, vilivyotolewa na Benki ya CBA Tanzania
kwa kushirikiana na Taasisi ya
Doris Mollel kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa
kabla ya wakati (Njiti).
Waziri
wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki
pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki
ya CBA Tanzania, Julius Konyani, wakimjulia hali mtoto Amani John
aliyelazwa katika wadi ya watoto ya Hospitali ya Wilaya ya Same, Mkoani
Kilimanjaro aliyepata ajali ya kuungua na moto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...