Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
CHAMA cha waajiri Tanzania (ATE) wameanza kutoa mafunzo ya kundi la tatu kwa wafanyakazi wa kike ikiwa ni programu ya mwanamke wa wakati ujao (Female Future) wakishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation Of Norway Enterpise NHO) kwa ajili ya kuboresha ufanisi kwa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yatakayokuwa katika kozi tatu yanalenga zaidi katika kuwapa mwongozo bora wafanyakazi wa kike ili waweze kumudu nafasi zao za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa wameshasajili wafanyakazi wa kike 24 kutoka makampuni 11 ambayo yamefadhili mafunzo hayo na kundi hili ni la tatu toka waazne kutoa mafunzo hayo na tayari wanawake 60 wameweza kupata programu hiyo.
Dkt Mlimuka amesema mafunzo haya yatachochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya kampuni na yatawapa ujasiri wanawake kuomba nafasi za uongozi sehemu mbalmbali ikiwemo bodi ya wakurugenzi..
Amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano na katika maisha yao kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (
ESAMI) kwa muda wa siku 14 muda wa darasani kwa kozi zote tatu ndani ya miezi tisa na yatafanyika kwa mfumo wa kuunganishwa na shughuli za kila za muhusika mahali pake pa kazi.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya mwanamke wa wakati ujao (Female in future) yenye malengo ya kumpa fursa mwanamke
juu ya uongozi, ufanisi katika bodi, ufanisi katika mawasiliano
wakati akizindua leo Jijini Dar es Salaam. Chini akizungumza na wanahabari.
Mhadhiri mwandamizi wa
Taasisi ya Usimamizi wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Apollonia Kerenge akizungumza na wanawake waliokatika mafunzo ya mwanamke wa wakati ujao (female in future) iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akiwa katika picha ya pamoja na wanawake walioko katika mafunzo ya proramu ya wanawake wa wakati ujao (female in future) iliyozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...