Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeahidi kuipanua zaidi kampeni yake ya ‘Happy Hour’ inayoendelea katika vituo vyake vya mafuta vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kuwafikia wateja wa kampuni hiyo kote nchini kufuatia muitikio mkubwa ulionyeshwa na wateja katika kuipokea kampeni hiyo.

Kampeni hiyo ambayo kwa sasa inahusisha vituo vya mafuta vya Puma vilivyopo vilivyopo mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, inamuhakikishia mteja rejesho la asilimia 5 ambalo ni sawa na Tsh 100 kwa kila Tsh 2,000 atakayotumia kununua mafuta kwa njia ya simu za mikononi au akaunti ya benki kupitia huduma Masterpass QR katika siku zote saba za wiki kuanzia saa 10:00 hadi 12:00 jioni.

Akizungumza kupitia taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw. Philippe Corsaletti amesema kwa sasa wateja wa kampuni hiyo wanaweza kufanya malipo kwa urahisi, haraka na kwa usalama zaidi kwa kutumia pesa zilizopo kwenye akaunti zao za simu au akaunti za benk.

“Kupitia kampeni hii tunashuhudia wateja wetu wakihamia kwenye ulimwengu wa kidigitali zaidi na kuungana na wenzao wengi ulimwenguni ambao tayari wapo huko. Aidha, ili kufanikisha hili tumewajengea uwezo wahudumu wetu waliopo kwenye vituo vyetu na sasa wapo tayari kuwasaidia wateja watakaopatwa na changamoto ya aina yoyote katika kufanikisha miamala yao,’’ alifafanua.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...