Na Robert Hokororo, Kishapu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imejipanga kufanya vizuri katika
ukusanyaji mapato ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 14, 2018 na Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha
Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka
2017/2018.
Alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia kwa wataalamu
wake imeweka mikakati thabiti kuhakikisha inafika maeneo yote na
kukusanya mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali.
“Zipo dalili za kufanya vizuri katika ukusanyaji katika mwaka huu mpya wa
fedha ingawa bado kuna changamoto nyingi zinatukabili nawaomba
wataalamu msikate tamaa tuendelee kuchapa kazi ili tuwahudumie
wananchi,” alisisitiza.
Mhe. Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka
madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za
maendeleo zikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu iliweza kukusanya kiasi cha sh. Bilioni 25.1 kutoka
katika vyanzo vyake mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Bonophace
Butondo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za robo
ya nne ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Wajumbe wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...