Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi nchini wameaswa kutoa wataalamu wa maendeleo ya Jamii wenye viwango vya juu ili kuendana na ushindani uliopo na katika kufikiamuchumi wa kati na wa viwanda.
Hayo yamesemwa leo Mjini Singida na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni na utakaoanza kutumika kwa mwaka wamasomo 2018/2019 mpaka mwaka 2022/2023.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bw. Golwike amewapongeza wakuu wa vyuo na wakufunzi hao kwa kazi nzuri wanaoendelea kufanya katika kutoa wataalamu wenye viwango katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.
Ameongeza kuwa wakufunzi hao wanatakiwa kuongeza nguvu katika kutengeneza wataalamu wengi wenye viwango zaidi ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na ushindani katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.
“Tutengeneza wataalamu wenye viwango ili tuendane na mabadiliko hasa kuelekea uchumi wa viwanda” alisisitiza Bw. Golwike
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick
Golwike akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa Vyuo na
wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la
kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa
na NACTE hivi karibuni.
Mkurugenzi
Msaidizi upande wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka
akielezea lengo na umuhimu wa mafunzo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa
wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi
yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya
Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Mwenyekiti
wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bw. Paschal Mahinyila akitoa
salamu za Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa Mwakilishi wa Katibu
Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike
wakati wa uzinduzi wa mafunzo wa wakuu kwa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala
mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Mwakilishi
kutoka NACTE Bw. Gidion Karuguru akitoa muongozo wa matumizi ya Mtaaka
Mpya kwa Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi wakati wa
uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo
ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Wakuu
wa Vyuo na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini
wakifuatilia mafunzo ya Mtaala mpya kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na
Ufundi nchini uliopitishwa na NACTE hivi karibuni utakaoanza kutumika
kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Picha zote na Kitengo cha Mawasilino
WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...