Mtaalamu wa masuala ya Jinsia, Bajeti kwa Mtazamo wa kijinsia na Haki za
Binadamu, Ndg. Gemma Akilimali (aliesimama) akitoa mada kwa Wajumbe wa
kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti katika semina iliyofanyika leo
katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia mada
iliyowasilishwa na Mtaalamu wa masuala ya Jinsia, Bajeti kwa Mtazamo wa
kijinsia na Haki za Binadamu, Ndg. Gemma Akilimali (aliesimama) wakati
wa semina iliyohusu Bajeti kwa Mtazamo wa Kijinsia leo katika Ukumbi wa
Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George
Simbachawene (kushoto) akizungumza jambo wakati kamati hiyo ikipatiwa
semina iliyohusu Bajeti kwa Mtazamo wa Kijinsia, leo katika Ukumbi wa
Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe.
Husna Mwilima. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...