Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

KATIKA hali ya kustaajabisha mkazi mmoja katika kijiji cha Magoza Wilayani Mkuranga amemuua mkewe na kumfukia.

Imeelezwa kuwa katika  kijiji cha magoza  Kata ya Kiparang'anda Wilayani Mkuranga  Selemani Juma amemuua mkewe Bi Selina Sulubu kwa madai ya mgogoro wa mapenzi uliodumu kwa muda mrefu na kisha kumfukia kwa siri katika shamba la jirani yake.

Tukio hilo limebainika leo baada ya siku kumi kupita tangu kufukiwa kwa mwili huo.

Michuzi blog ilifika eneo la tukio na kushuhudia jeshi la polisi kwa kushirikiana na wataalam wa afya  kutoka hospitali ya Wilaya na wananchi wakifukua mwili wa marehemu.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkuranga Dkt. Steven Mwandambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  kwa kuuona mwili wa marehemu na wamekabidhi jeshi la polisi ili waweze kuendelea na hatua nyingine.

Aidha kaka wa marehemu  bahati Mabubu amesema; baada ya kupata taarifa kwa shemeji yake kuhusu kutoroka kwa dada yake nyumbani aliamua kufunga safari kuja Mkuranga ili kumtafuta dada yake.

Mabubu ameongeza kuwa alipofika Mkuranga katika kijiji cha magoza alibaini shemeji ya kuwa na hali ya wasiwasi,ndipo alipompeleka kituo cha polisi na kukiri kufanya mauji ya mke wake.

Ikumbukwe kuwa ni miezi minne tu imepita tangu kutokea kwa mauaji ya nesi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga yaliyosabishwa na wivu wa mapenzi kutoka katika wilaya ya Mkuranga.
Polisi na wataalamu wa afya kwa kushirikiana na wananchi wakisaidiana kufukua mwili wa Selina Sulubu aliyeuwawa na mumewe katika kata ya Kiparang`anda Wilaya ya Mkuranga mkoa Pwani. (picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Polisi,wataalamu wa afya kwa kushirikiana na wananchi wakibeba mwili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...