WIZARA ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), kwa kuchukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa wa
Ebola usiingie nchini, imeelezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri
wa Wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu katika hotuba yake kwa wananchi
walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii
kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini yaliyoanzia kwenye viwanja vya Mnazi
Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo
imesharipotiwa ugonjwa huo umeingia nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasia
ya Kongo.
Mhe. Mwalimu amesema TAA inafanya
jambo jema kwa kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini kupitia
viwanja vya ndege wanafanyiwa ukaguzi na kutoa taarifa za afya zao kwa
wale ambao watabainika kuwa na joto la mwili lisilokuwa la kawaida.
“Nawapongeza sana tena sana
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa kuhakikisha nchi inakuwa
salama bila kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa Ebola, imeripotiwa sasa
huu ugonjwa upo Kivu Kaskazini, ambapo ni karibu na nchini na Wavuvi
wanakuwa na muingiliano kwa kutoka huko na kuja nchini,” amesema Mhe.
Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akiongea na wananchi walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...