NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 


WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeziasa halmashauri kuhakikisha zinapima maeneo ya wananchi na kuyaingiza kwenye mfumo ili kutambua idadi ya viwanja na mashamba wanayopaswa kulipa na kupatiwa hati miliki. 

Imetoa rai kwa halmashauri hizo kutotumia kigezo cha kutopewa fedha na wizara hiyo kwa ajili ya bando la kuweka katika mfumo kama kikwazo cha kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na ardhi. 

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Angeline Mabula.Alisema , suala hilo ni aibu kwa halmashauri kudai wanakosa kiasi cha sh. 20,000 ama 30,000 ya vocha . Angeline alieleza, halmashauri wasigeuze jambo hilo kama ni changamoto ya kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na ardhi na kusubiri kupewa na wizara wakati hilo liko ndani ya uwezo wao. 

“Mnakusanya mabilioni ya fedha kupitia viwanja mnashindwaje kukusanya mkiwa mnasubiri vocha ya shilingi 20,000 au 30,000 hili halikubaliki " 
Angeline alifafanua,, halmashauri zihakikishe zinawezesha idara ya ardhi iweze kukusanya mapato badala ya kuiacha kama mtoto yatima . 

“Tumerejesha maeneo mengi lakini nia njema ya kufanya hivyo baadhi halmashuri zimekiuka mnaweza kuwa na kasi ya kutaka maendeleo lakini unapaswa kufuata taratibu hatuwezi kutoa maeneo bila kufuata taratibu,” alisema Angeline. 

Ofisa ardhi mteule wilaya ya Kibaha ,Majaliwa Jafari alieleza viwanja 1,700 vimepimwa lakini havijauzwa ambapo Kisabi 800 Disunyala 700 . Awali akisoma taarifa ya wilaya katibu tawala wa wilaya hiyo Sozi Ngate alisema , halmashauri ya wilaya ilikusanya milioni 504 na kutoa hatimiliki za kimila na imepima vijiji 22. 

Anasema, mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi umegusa maeneo tisa kati 25 vilivyopo ikiwemo Lukenge, Gumba, Magindu, Mpiji Station, Kwala, Dutumi, Minazimikinda, Mperamumbi.
 Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama akizungumza wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akieleza jambo, wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha.
Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula ( wa katikati) akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama (wa kwanza kulia )wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha, (wa kwanza kushoto) ni mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...