Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kipindi kipya chenye mahadhi ya pranks (kumstua mtu huku ukimrikodi anavyostuka, bila yeye kufahamu), kinaanza mwezi Oktoba. 
 Katika mahojiano maalum na mwasisi na mendeshaji wa kipindi hicho, mwanahabari wa kimataifa wa Tanzania Joseph Msami, ambaye hivi karibuni alikuwa mtayarishaji wa vipindi wa Idhaa ya Kisahili ya Umoja wa Mataifa mjini New York, amesema STUKA ni kipindi amabacho kitawaelimisha watanzania kaika Nyanja mbalimbali kama za kijami, kiuchumi kwa kutumia mbinu za burudani. 
 Msami amesema kipindi hicho ambacho hutumia mbinu ya kamera isiyo hadharani na kuwanasa wakazi katika pitapita zao za kila siku, hakimlengi mtu maalum wala kumuandaa yeyote (Reality Show) na kitatoa burudani ya kutosha kutokana na maadalizi yaliyofanywa na timu ya STUKA kwa zaidi ya miezi mitatu. 
 Amesema timu hiyo inayojumuisha wataalamu wa maudhui ya habari, picha na sauti imekuwa katika mafunzo maalum yaliyolenga kuhakikisha umma unapata elimu na burudani kwa kuzingatia weledi. Kipindi chicho kitakachorushwa na kituo cha televisheni ya TVE katika muda ambao watazamaji wengi huangalia runinga (Prime Time ), na kurudiwa mara kadhaa ili kutoa fursa kwa watazamaji kuona uhondo huo kwa wingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...