BENKI ya NMB Plc imesema itaendelea kusaidia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari jana katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaoendelea jijini Dodoma, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, amesema benki yake imetengeneza program mbalimbali za kusaidia kuchochea kasi ya uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Hata hivyo, amesema, benki ya NMB ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 31, ni miongoni mwa taasisi chache za fedha hapa nchini zinazofanya kazi kwa ukaribu sana na Serikali.“Kwa mfano, NMB imekuwa mdhamini mkuu wa mikutano mikuu ya ALAT miaka sita sasa, na kwa mwaka huu, benki imetoa udhamini wa shilingi milioni 100. Hii inaonyesha utayari wetu katika kufanya kazi pamoja na Serikali,” alisema.

Aidha, amesema NMB inafanya kazi pamoja na wilaya na halmashauri zote nchini, ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo rafiki kwa wafanyakazi wa Serikali.“Lengo ni kuhakikisha huduma za kifedha za NMB zinawafikia Watanzania wote nchini hususani wale wanaoishi katika jamii za vijijini ambapo kunachangamoto nyingi za kimaisha na kiuchumi,” alieleza.

Amesema kwa sasa benki imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kutoa mikopo rafiki kwa wajasiliamali wa kati na wadogo nchini, lengo kuu likiwa ni kuchochea uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo na mifugo.“Uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya kilimo na mifugo na hivyo, NMB itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo kupata mikopo nafuu na rafiki ili waweze kujikita katika miradi husika,” aliongeza.
Wajumbe wa Mkutano Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakishiriki mkutano huo ndani ya ukumbi wa mikutano wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma- mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya NMB. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakipata maelezo walipotembelea banda la Maonesho la Benki ya NMB Ukumbi wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma jana- mkutano huo umedhaminiwa na benki ya NMB.

Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma jana kwenye Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) unaoendelea Jijini hapo. Mkutano huo unaoshirikisha zaidi ya washiriki 500 kutoka Halmashauri, Wizara na Idara mbalimbali za Serikali umedhaminiwa na benki hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...