JOSEPH MPANGALA, MTWARA
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa mafunzio kwa
Wafanyabiashara wa Mkaoni Mtwara kuhusiana na Msamaha wa Riba na adhabu ya
malimbikizo ya Madeni ya kodi kwa lengo la kuwawezesha wafanyabishara hao
kuweza kutambua masuala yanayohusu Kodi pamoja na kuwahi Kuomba Msamaha wa Riba
na Adhabu zake.
Akifungua mafunzo hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara
Evod Mmanda,Katibu Tawala Msaidizi wa
Mkoa wa Mtwara Renatus Mongogwela amesema
katika kipindi kirefu walipakodi wengi walikuwa wanashindwa kulipa Kodi zao
kikamilifu kutokana na kuelemewa na malimbikizo makubwa ya Madeni yaliyotokana
na Riba na Adhabu.
“Nipende Kuwafahamisha Kuwa Serikali imesikia kilio cha Walipa
kodi na kuweka taratibu maalim wa kuyaondoa hayo malimbikizo ya madeni ya
riba,hivyo niwasihi ndugu zangu tutumie fursa hii adhim kuweka sawa masuala
yenu ya kikodi na kupitia Msamaha huu Serikali inaaamini walipa kodi wataanza
upya kuzifuata na kuzitii Sheria hizi”amesema Mongogwela.
Mafunzo hayo ya Siku moja yamejumuisha mabadiliko ya Sheria
ya kodi ya mwaka 2018 pamoja na mfumo wa
maadili wa watumishi wa mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA} kwa lengo la
kuwawezesha wafanyabiashara kuweza kutoa
maoni na kapata huduma Bora.
Katibu Tawala Msaidi wa Mkoa wa Mtwara Renatus Mongogwela
akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania {TRA} juu ya
elimu ya Msamaha wa riba na adhabu kwa wanyabishara wa Mkoa wa Mtwara.
Afisa maadili mwandamizi Mika Kiremera kutoka mamlaka ya mapato Tanzania {TRA}makao
makuu akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi pamoja na maadili
kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mtwaa.

Msimamizi wa Shule ya Sekondari Aquinas Sister Paula
Ngagani akiongea na Afisa Mkuu wa elimkwa Mlipa Kodu Makao Mkauu Julius Ceasar
pamoja na Meneja wa Mamlaka ya mapato mkoa wa Mtwara Naomi Mwaipola mara baada ya kumalizika kwa
mafunzo ya TRA kwa Wafanyabiashara Mkoa wa Mtwara.

Baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria Mafunzo
yaliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania {TRA}Mkoani Mtwara kwa lengo la
kutoa elim ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya
Kodi,mabadiliko ya sheria ya kodi ya mwaka2018 pamoja na Maadili.
Wafanyabishara Mkoa wa Mtwara wakiwa pamoja na maafisa wa
mamlaka ya mapato Tanzania TRA mara baada ya Kumalizika kwa mafunzo ya siku
moja kuhusina na elimu ya Msamaha wa Riba na adhabu pamoja na maadili kwa
watumishi wa TRA>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...