Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki maonyesho ya
kwanza ya madini yanayoendelea mkoani Geita kwa lengo la kuwafikia kwa
ukaribu zaidi watanzania wote watakaoshiriki maonyesho hayo kwaajili ya
kutoa elimu na kuandikisha.
Maonyesho hayo ambayo yameshirikisha wadau wote wa sekta ya madini
yameanza Septemba 24 hadi Agosti 30 2018 katika viwanja vya
kalangalala mkoani Geita.
Kufuatia mabadiliko ya sheria, NSSF sasa inalenga kuandikisha wale wote
waliopo sekta binafsi ya ajira na sekta isiyo rasmi, ili wanufaike na
mafao yatolewayo na shirika hilo ikiwemo fao la matibabu bure kwa
mwanachama na familia yake.
Akizungumza leo kutoka viwanja vya kalangalala Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita
Bwana Shaban Mpendu ametoa wito kwa watanzania wote kutembelea maonyesho
hayo ya migodi na kufika katika banda la NSSF ili kuweza kupata elimu
ya mafao yanayotolewa na NSSF pamoja na elimu ya hifadhi ya jamii kwa
ujumla.
Vilevile meneja amewataka wananchi hasa wa sekta binafsi na
sekta isiyo rasmi kujiandikisha na NSSF. Uandikishaji unaofanyika katika
banda la NSSF ni pamoja na uandikishaji wa waajiri, wanachama na
usaijili wa matibabu bure.
Meneja wa NSSF mkoa wa Geita akimkaribisha mgeni rasmi Mh Stanslaus
Nyongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika banda la NSSF kwenye
maonyesho ya kwanza ya madini mkoani Geita
Meneja wa NSSF mkoa wa Geita Shaban Mpendu akitoa elimu kwa wadau
wa sekta ya madini juu ya huduma zitolewazo na nssf katika maeonyesho
ya kwanza ya madini yanayoendelea mkoani geita
Afisa
mafao wa NSSF mkoa wa Geita bi Annastazia Ngallaba akimjazisha fomu ya
uandikishaji mdau aliyetembelea banda la nssf kupata elimu na kuelewa
somo hatimaye akaamua kujisajili.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stanslaus Nyongo akipewa maelezo
kwa ufupi katoka kwa Meneja wa NSSF Geita Ndugu Shaban Mpendu juu ya
huduma zitolewazo na NSSF alipotembelea banda la NSSF muda mchache kabla
ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...