Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA)  imesema kuwa viwanja vya ndege na wadau wengine katika usafiri wa anga wanatakiwa kuwa na mikakati ya kukubiliana na magonjwa ya kuambukiza ili kufanya usafiri wa anga kuwa salama kwa abiria pamoja na mizigo.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa usafiri wa anga uliofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka hiyo  , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Redemptus Bugomomola amesema viwanja vya ndege vinatakiwa kuwa na huduma za Afya kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza ili kuweza kulinda jamii kutoka sehemu kwenda nyingine.

Bugomola amesema kuwa baada ya kuwepo magonjwa ya kuambukiza kwa watumiaji usafiri wa anga Shirika la Usafiri wa Anga (ICAO) liliunda chombo cha kuratibu masuala kukabiliana na magonjwa ya  kuambukiza katika Viwanja vya Ndege CAPSCA  ambapo nchi za Afrika bado ziko nyuma katika kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza.

Amesema kuwa TCAA kwa kushirikiana na wadau kunahitajika kuwepo na mikakati ya kila mmoja kutambua umuhimu wa kufanya kazi katika kukabiliana magonjwa ya kuambukiza kutoka ndani au kwenda nje pamoja na wa nje kuangalia wasiweze kuambikiza wanapingia nchini.

Nae Mkuu wa Vituo vya Afya Mipakani wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Remidius Kakula amesema kuwa kupitia ICAO  imeweka viwango vya viwanja vya ndege kuwa mazingira ya kuweza kukabiliana na maginjwa ya kuambikiza.

Amesema kuwa kila kiwanja cha ndege kinatakiwa kuwa na chumba maalumu pale anapobainika kuwepo kwa mgonjwa ili kuweza kupata huduma haraka ndani ya  uwanja ndege ikiwemo na huduma ya Thermo ya kupima kiwango cha joto pamoja na kuwa gari ya wagonjwa kwa kila kiwanja cha ndege..

Amesema katika mkutano huo watajadiliana mbinu mpya ya kukabiliana magojwa ya kuambukiza kwa magonjwa yaliyotishio kama vile Ebola , Homa ya Ini, Mafua ya Nguruwe pamoja na Mafua ya Ndege.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Redemtus Bugomola akizungumza katika mkutano wa wadau wa anga kuhusiana na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika viwanja vya ndege uliofanyika katika ukumbi wa TCAA, jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Daniel Malanga akizungumza kuhusiana na masuala mbalimbali ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza katika viwanja vya ndege.
Baadhi ya wadau wa usafiri wa anga katika mkutano wa kujadilia namna ya kukabiliana na magonjwa kuambukiza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...