Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watu
walionusurika katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere wakati
alipotembelea Kituo cha Afya cha Bwisya kisiwani humo Septemba 24,
2018. Wengine ni mwananchi ambao bado wamepotelewa na ndugu na jamaa
katika ajali hiyo wakisubiri kutambua miili endapo itaonekana.
Gari la wagonjwa likiwa limeegeshwa kwenye jengo la Kituo cha Afya cha
Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukererwe ili kuteremsha mwili
wa mtoto ambao waokoaji waliupata katika kivuko cha MV Nyerere
Septemba 24, 2018. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kituo hicho
leo asubuhi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akikabidhi kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isaack Kamwelwe mchango wa sh.
milioni 10 zilizotolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia katika ajali ya
Kivuko cha MV Nyerere kilichozama ktika kisiwa cha Ukara wilayaniu
Ukerewe, Septemba 20, 2018. Makabidhiano hayo yalifanyika katika
kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara, Septemba 24, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali, Venance Mabeyo baada ya kumkabidhi jukumu kuwa msimamizi mkuu
wa operesheni ya uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye
kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 24,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu,
Jenista Mhagama (katikati) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Profesa Faustine Kamuzora kwenye kijijii cha Bwisya katika kisiwa cha
Ukara wilayani Ukerewe baada ya Waziri Mkuu kutembelea eneo kilipozama
kivuko cha MV Nyerere kijijini hapo Septemba 24, 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...