WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amempongeza Rais wa China Xi Jinping kwa mikakati mbalimbali kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika aliyotangaza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Serptemba 05, 2018) alipokutana na Meya wa Manispaa ya Shenzhen na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China wa Jimbo hilo Wang Wanzhong  katika hoteli ya Wu Zehou  iliyoko  Shenzhen.

Amesema anampongeza Rais Xi kwa kutangaza mkakati wa kuimarisha ushirkiano na nchi za Afrika kwa sababu Tanzania nayo itaendelea kunufaika zaidi kupitia mipango na mikakati hiyo. Waziri Mkuu amesema licha ya asilimia 70 ya Watanzania kutegemea kilimo katika kuendeshaji wa maisha yao, Serikali imeamua kuboresha uchumi wa nchi kupitia  sekta ya viwanda  hususani vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Hivyo, inahitaji washirika wengi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kuboresha uchumi kupitia viwanda. Mkakati wa kuwekeza katika viwanda unatoa fursa kwa Watanzania na watu kutoka nje ya nchi ikiwemo China kuja kuwekeza.” 

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wakezaji kutoka Manispaa ya Shenzhen  waje wawekeze kwenye maeneo mbalimbali nchini kama uchimbaji na uchakataji wa madini hususani ya Tanzaniteili kuiwezesha nchi kunufaika na madini hayo yanayopatikana  Tanzania tu. Waziri Mkuu amesema anaamini kuwa miji mbalimbali Tanzania inaweza kufikia maendeleo ya viwanda yaliyofikiwa na mji wa Shenzhen katika  kipindi cha miaka 38 tangu kuanzishwa kwa mji huo kama eneo la kwanza la kiuchumi.

“Nawakaribisha wawekeze kwenye sekta ya teknolijia ya habari na mawasiliano nao waje nchini kama ilivyofanya kampuni ya HUAWEI ya Shenzhen  ambayo inafanya kazi nzuri na kutoa mchango mkubwa kwa sekta hiyo nchini kwetu.”

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Wang  amemshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kutembelea Shezhen na kwamba  Shenzhen itaitikia wito wa Rais Xi  wa kushirikiana na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya uchakataji mazao ya kilimo. Kuhusu uwekezaji wa viwanda, kiongozi huyo aliahidi kuwasiliana na EPZA kuona namna bora ya kushirikiana na Tanzania . Aidha aliahidi kutuma ujumbe nchini kutoka Shirikisho la Wasanifu na Watengenezaji Vito vya Madini waje waangalie namna ya kushirikiana na Tanzania hususani katika madini ya Tanzanite.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea Kampuni ya Huawei Technologies, Kituo cha Sanaa na Makumbusho cha Sea World na Kampuni ya China Merchant ambayo ina mpango wa kuwekeza kwenye mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...