Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imetoa ripoti ya matukio  ambayo ni mkakati wa kitaifa dhidi ya rushwa na mpango wa utekelezaji wa awamu ya tatu  unaoratibiwa na kitengo cha uratibu wa utawala bora ofisi ya Rais Ikulu katika kupiga vita vitendo vya rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa aliyekuwa mkurugenzi  mtendaji wa taasisi ya PRIDE  inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wananchi hasa akina mama ili kuwainua kiuchumi Rashid Malima (60) anatafutwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.
Amesema kuwa taasisi hiyo iliundwa kwa lengo la kusaidia wananchi wenye kipato kidogo na ilipata mtaji wake wa kwanza wenye thamani ya dola za kimarekani 4,000  kutoka Norway  kupitia NORAD.
Mbungo ameeleza kuwa katika vipindi mbalimbali kati ya mwaka 2015/2017 Malima na wenzake walifanya ubadhilifu wa fedha za kampuni ya PRIDE za kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni nane  na kuandaa malipo hewa kwa watoa huduma mbalimbali yakiwemo Arusha Art, Antelop Safaries, Essence international na paperwork na pia waliandaa malipo ya salary advance ambayo hayakufuata taratibu na baadaye fedha hizo zote walizichukua na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.
Aidha amesema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutoroka nchini punde tu uchunguzi wa tuhuma hizo ulipoanzishwa mwaka 2018 na taarifa zilizopo ni kwamba alitoroka kupitia eneo la Namanga, na inasemekana kuwa yupo nchini Marekani hivyo amewaomba watanzania nchini na wale wanaoishi Marekani kutoa taarifa za mtuhumiwa huyo ili sheria ifuate mkondo wake.
Naibu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutafutwa kwa watuhumiwa waliokimbia baada ya kutenda makosa ya rushwa, wizi na ubadhilifu wa fedha za umma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...